Written by Jeremy Kabiru

Tumetoka mbali si wakenya, twaenda mbali zaidi

Miaka zaidi ya hamsini na tano, hatua twaendelea kuchukua

Twajivunia uzalendo, kabila tofauti kuungana

Daraja hatujamaliza kuvuka, hatujidanganyi tumeshafika

 

Kujenga taifa letu, kwetu wakaaji faidi

Tumechukua hatua, zaidi ya moja twajua

Rabani twaomba leo, ikuwe bora kuliko jana

Kwa kushirikiana tutapenya, tukijitenga tutajibana

 

Tukikumbuka wakati wa kale, wengi walipigania uhuru

Kujikomboa kutoka mababe, si jambo kidogo wala rahisi

Tuliobaki tuichunge na tuilinde, taifa letu bado changa

Tujipende na tuipende, siasa isiwe ikatutenganisha

 

Shida ukweli ni nyingi, kama wangwana tutafute suhulu

Masomo ni muhimu, kujikomboa kazi yetu sisi

Tusirudie yaliyopita, kuchukulia wenzetu mishale ama panga

Kenya ni yetu sote, tujinufaishe tujiboreshee maisha

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.